Jana
ndipo ilipokuwa safari ya mwisho ya Marehemu Mzee Sykes baba yake na
Msanii Mkongwe Nchini Dully Sykes (@dully_sykes) ambapo Mzee Sykes alipumzishwa katika
makazi yake ya Milele huko katika Makaburi ya Kisutu Jijini
Dar-es-Salaam.
Kutokana na Msiba huo Tokea Juzi simu ya Dully Imekuwa haipatikani Ila leo @DjHaazu wa @MamboJamboRadio amempata na Kupiga naye Story mbili tatu kuhusiana na Marehemu Mzee Sykes kwa kifupi.
Katika
Mazungumzo yake Dully ameeleza kuwa Mzee Wake alikuwa anaugua Muda
mrefu na kilichopelekea kifo chake ni uvimbe Miguuni ambao ulipelekea
Kutengeneza sumu mwilini na Hatimaye kupelekea Sumu hiyo kuzima Taa
Angavu.
Matumizi ya Sigara nayo Amesema ni Chanzo cha Kifo cha Mzee Sykes japo ameugua ile Serious kwa wiki Mbili.
Kwa
upande M,wingine Dully amesema kuwa Tofauti na Damu ya Mzee Kumzaa
lakini Baba yake ana mchango Mkubwa sana Katika Maisha yake ya Muziki na
Ana nafasi kubwa sana ya Pale Dully alipo hadi leo hii.
No comments:
Post a Comment
paulmkale