Diamond asitisha kupokea maombi ya collabo za wasanii wa Nigeria

Diamond Platnumz nae kuna kingine kutoka kwake leo, jamaa kasema ameamua kusimamisha kufanya collabo na wasanii wa nje kwa kuwa mara ya kwanza alizipiga nyingi ili kutafuta upenyo mzuri Afrika ijue muziki mzuri wa TZ.. YES, kapiga kazi nyingi na mastaa wengi na hiyo imeuweka muziki wa TZ mahali pazuri, kwa sasa collabo hizo zitasimama.
Diamond amesema collabo ya mwisho kufanya kwa sasa itakuwa ya yeye na K Cee, staa kutoka Nigeria.
Diamond anasema japo kaamua hivyo lakini kuna foleni ya mastaa ambao nao wameomba nae collabo mpaka sasa wengine hata hawakumbuki majina yao !!

No comments:

Post a Comment

paulmkale