Huwa ni mara chache sana utasikia staa au mtu maarufu kajitokeza au
kakubali kuweka wazi kuhusu sehemu aliyowahi kuharibu au kufeli kwenye
maisha.
Kwenye muziki wa bongofleva tunae Nuh Mziwanda ambaye pia ni boyfriend
wa msanii Shilole…… Nuh ameongea ukweli wa moyoni kwenye exclusive
interview na millardayo.com na kusema >>> ‘Kwenye
maisha yangu ninachojutia ni nilivyofeli mtihani wangu wa form IV
nilipata Zero kabisa na sikufanya mitihani kama mitatu, yote hiyo
ilitokea sababu ya muziki’
‘Nilikua
mtoto mwenye akili sana na Mama yangu alikua anategemea nitakuja kuwa
mtu flani mwenye elimu yake kwenye familia yetu na sio Mwanamuziki,
nyumbani kwetu tuko watano na mimi ndio wa mwisho na nilikua nina akili
sana kuliko wote na kuanzia la kwanza mpaka la saba nilikua sishuki
kwenye Wanafunzi kumi bora‘
Kwenye sentensi nyingine Nuh anamalizia >>> ‘Kupata
Zero Form IV ni jambo ambalo linanifanya nijute sana mpaka sasa,
ningekaza ningekua nafanya muziki huku nikisoma lakini nilivyojua
maswala ya muziki tu nikaachana na Masomo, najutia…. nilikuja nikarudia
tena mitihani na nikafeli, inaniuma sana… kama ninavyokosea kiingereza
sio kwamba napenda, ni shule hamna’
Nuh amesema kuna uwezekano wa kurudi shule >>> ‘shule
ni kitu muhimu haikataliwi, ni kitu poa unakuwa Mwanamuziki alafu una
elimu yako… na muziki naudai sana ndio maana naukazania sababu
ulinifanya nifeli shule’
No comments:
Post a Comment
paulmkale