“Nana” ya Diamond na “Chekecha” ya Ally Kiba katika Top 10 ya Radio maarufu ya Nigeria.
Muziki wa Tanzania unaendelea kufika mbali zaidi kwa kutoa wasanii wakubwa wanaofanya vizuri kama Diamond Platnumz. Ally Kiba ni mmoja ya wasanii kutoka Tanzania ambae anafanya vizuri kwa sasa na nyimbo yake ya Chekecha.
Nyimbo ya Chekecha inaendelea kufanya poa Afrika baada ya kuingia katika Top 10 za Radio maarufu ya Nigeria iitwayo THE BEAT 99.9FM, chekecha katika wiki hii imeshika nafasi ya tisa.
Katika chart hiyo ya “Nana” ya Diamond aliyomshirikisha Mr Flavour imekamata nafasi ya pili katika wiki hii…Big up Ally Kiba na Diamond Platnumz kwa kuendelea kutuwakilisha vizuri kimataifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
paulmkale