Salama Jabir: Ally Kiba hana Matatizo na Diamond Platnumz, Wakikutana Wataongea..

Kumekuwa na Mvutano mkubwa sana baina ya Team mbili kati ka Team Diamond na Team Kiba, Salama Jabiri kaongelea hizi Timu na Kusema Kuwa hadhani kama Diamond na Ally Kiba wana Uadui mkubwa kama watu wanavyofikiria.Akiongea katika kipindi cha XXL Salama Jabiri amesema:
"Mimi na Ali Kiba sio Maadui pia mimi na Diamond Sio Maadui, sipendi jinsi ambavyo nikiongea na Diamond watu wanahisi mimi ni team Diamond na nikiongea na Ali Kiba wanasema mimi ni team Ali Kiba, Sina Team mi ni Mtanzania napenda mziki na wananikwaza sana kunitaka niwe upande Flani, siwezi kuwa upande flani , Diamond anajua kwamba mimi naongea na ali kiba, Ali Kiba anajua kuwa naongea na Diamond" aliongea Salama Jabiri.

Pia aliongeza"Am sure Ali Kiba hana matatizo na Diamond, na Diamond hana Matatizo na Ali Kiba hata kama wanayo ni kikazi ambapo wakikutana wataongea, tusiwawekee watu maneno kwenye midomo"

No comments:

Post a Comment

paulmkale