Ali Kiba atoa tsh 21Milioni na Diamond atoa tsh 20Milioni jumla tsh 41milioni kusaidia ‘GSM Foundation’ Bofya kujua zaidi
Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhawani Kikwete amewapongeza wasanii wa
muziki, Diamond Platnumz na AliKiba kwa kutoa msaada wa tsh 41milioni
kwa ‘GSM Foundation’ ili kusaidia jitihada za taasisi hiyo za upasuaji
wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Mtoto huyo wa Rais mtaafu, amewapongeza wasanii hao kwa kuonyesha kuguswa na kusaidia matatizo ambayo yanatokea katika jamii.
“Katika vitu vimeonyesha umuhimu wa kuwa stars katika jamii yetu ni
hili mlilolifanya wadogo zangu. Ni jambo la kusifiwa na Mungu atawalipa
kwa kuwaongezea maarifa ya kufanya kazi zenu vizuri,” Ridhiwani
aliandika katika instagram yake.
Aliongeza, “Pia niwapongeze sana GSM Foundation kwa kazi nzuri
mnayoifanya. Kutoa si utajiri, ni moyo na mungu atakuzidishia ndugu
mkurugenzi Gharib pale ulipotoa. Kila la kheri katika kusaidia jamii
yetu yenye mahitaji. Peace to you,”
Siku chache zilizopita Diamond Platnumz alitoa msaada kwa taasisi
hiyo wa tsh 20 Milioni na baadae AliKiba na yeye aliamua kutoa tsh 21
Milioni.
No comments:
Post a Comment
paulmkale