Watu Wa Africa Magharibi Wazuiwa Kuingia Kweye Nchi Hii
Serikali ya Australia imetengaza kuzuia
kuingia mtu yoyote anayetokea nchi za Afrika Magharibi zilizoathiriwa na
Ebola, Guinea, Liberia na Sierra Leone kama njia ya kujikinga na hatari
ya kuingia kwa ugonjwa huo nchini humo.
Mbali na taarifa iliyotolewa na chama
cha madaktari Australia (AMA) iliyosema kuwa nchi hiyo haiko kwenye
hatari ya kupatwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo, waziri wa
uhamiaji Scott Morrison ametangaza utaratibu ‘mgumu’ kwa mtu yoyote
anayetoka Afrika Magharibi kuingia nchini humo.
Akiongea katika bunge la nchi hiyo,
Morrison amesema kwa sasa wanasitisha maombi yote ya vibali vya kuingia
nchi hiyo kwa mtu yoyote anayetokea Afrika Magharibi, na kwa yeyote
mwenye hati ya kudumu ya kuingia nchini humo, unaandaliwa utaratibu wa
kuwapo sheria itakayowalazimu kukaa karantini ndani ya nchi wanakotoka
kwa takribani wiki 3 kabla ya kuanza safari ya kwenda Australia.
Kwa upandee wake waziri mkuu wa
Australia, Tony Abbott amesema hakubaliani na taarifa ya chama cha
madaktari inayosema Australia haiko katika hatari ya kupata maambukizi
ya Ebola, na kukosoa kuwa taarifa hiyo haijazingatia maslahi ya taifa
hilo.
Baadhi ya wabunge wa upinzani wamekosoa
maamuzi ya serikali ya nchi hiyo kwa kusema kitendo cha kuzuia watu
wanaotokea Guinea, Liberia na Senegal wasiingie nchini humo hakioneshi
picha nzuri ya taifa hilo.
No comments:
Post a Comment
paulmkale